ONYO: USIKUBALI KWENDA MIKOA HII. MKE USIRUHUSU MUMEO AENDE. MIMI TANGA NA TABORA SIENDI TENA
Wadau, Kutokana na mikasa mingi ambayo nimewahi kuipata na pia kusikia kwa ndugu, jamaa na marafiki nawashauri sana kuna mikoa msikanyage kabisa hizi ni story za kweli na nimezikatisha sana ili isiwe kero kwa wavivu wa kusoma kwa waliokuwa ndugu zangu hasa wale ambao wanatumia vichwa vidogo kufikiri. Mikoa hiyo ni Tanga, Tabora, Mtwara, Singida, Pwani katika hiyo mimi nimetembelea mikoa ya Tanga, Mtwara, Pwani na Tabora. Safari yangu ya kwanza kikazi nilipangiwa Mtwara miaka ya nyuma kidogo mwaka 2001 nilipokelewa huko na mwenyeji wangu akanipokea nlifikia kwake nikiwa nafanya utaratibu wa kutafuta kwangu ilikuwa wilaya ya Masasi, siku za mwanzoni kwa kweli sikuwa na kukurukakara nyingi lakini katika pita pita zangu siku moja nikakutana na binti mzuri sana anauza korosho. Nilishangaa yule binti mzuri anauza korosho na mchangamfu sana hakuw...